http://www.vodacom.co.za/

Tuesday, November 22, 2016

RC MAKONDA Atoa agizo zito kwa mgambo,,,,,,,





KIUNGO MKABAJI CSKA APATIKANA NA TUHUMA ZA UTUMIAJI MADAWA YA KULEVYA,,,,,,,,,,


Kiungo mkabaji wa CSKA Moscow ya Russia, Roman Eremenko amefungiwa miaka miwili baada ya kubainika anatumia madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

Eremenko amepatikana na hatia hiyo baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen iliyopigwa Septemba 14, mwaka huu na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), limepitisha na kuitangaza adhabu hiyo.


Kutokana na adhabu hiyo, Eremenko raia wa Finland ataukosa msimu wote ujao pia utakaofuata nusu msimu.


Bodi ya Uefa ya Uthibiti, Hadhi na Nidhamu imesema itaendelea kufanya uchunguzi kama kawaida kwa wachezaji mbalimbali kama ambavyo imekuwa ikifanya.

HESHIMA KWAKE, ZLATAN IBRAHIMOVIC KUTENGENEZEWA SANAMU, LITAWEKWA NJE YA UWANJA,,,,,,,,,,,,,


Shirikisho la Soka la Sweden (SvFF) limetangaza kutengenezwa kwa sanamu maalum la mshambuliaji nyota wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic.
Zlatan ni mchezaji wa timu ya taifa ya Sweden na nahodha, lakini ni Mswidi aliyeshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa Sweden kwa miaka 10 mfululizo.
Sanamu lake litawekwa nje ya Friends Arena katika jiji la Stockholm.
Hali hiyo ni kuonyesha kuthamini mchango wake akiwa na timu ya taiga ya Sweden lakini kuwasaidia wanamichezo chipukizi kuhakikisha wakiwa na hamu ya kupata mafanikio.
Zlatan ambaye sasa ana umri wa miaka 36, akiwa na timu ya taifa ya Sweden amecheza mechi 114 na kufunga mabao 62. Alitangaza kustaafu baada ya michuano ya Euro iliyofanyika nchini Ufaransa, hivi karibuni.



TAKWIMU ZAKE
KLABU ALIZOPITIA: Malmo, Ajax, Juventus, Inter, Barcelona, AC Milan, PSG, Manchester United
MECHI: 646; 
MABAO: 381
MECHI TIMU YA TAIFA: 116; 
MABAO: 62

MAKOMBE: 2009/10 La Liga, 4x Serie A (Mara tatu akiwa na Inter, Mara moja na AC Milan), 4x Ligue 1, 2x Eredivisie, 2010 FIFA Club World Cup, 2010 UEFA Supercup

Baba wa Kambo Anajisi Mtoto Miaka Tatu, Amuua,,,,,,,,,,,,,,,

MTOTO mdogo mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Nyamihaga Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma amekufa baada ya kunajisiwa na baba yake wa kambo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kwamba wamemtia mbaroni mtuhumiwa Hamimu Saidi (27) mkazi wa kijiji hicho cha Nyamihaga.

Akitoa maelekezo kuhusu mkasa huo, Kamanda Mtui alisema mtuhumiwa alitekeleza dhamira yake hiyo wakati mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa mke wa mtuhumiwa alipokwenda kisimani kuchota maji.

Alisema baada ya mwanamke huyo kurejea nyumbani kutoka kisimani alimshuhudia mtoto wake akilalamika sana wakati akitaka kujisaidia haja ndogo na ndipo alipomchunguza akagundua kwamba mtoto huyo alikuwa ameingiliwa na kujeruhiwa kwenye sehemu zake za siri.

Kamanda Mtui alisema baada ya kugundua hilo, mama huyo wa mtoto alimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitali ya Mkoa ya Maweni kwa matibabu, ambako iligunduliwa kuwa mtoto huyo alikuwa amenajisiwa na alikuwa amebanwa shingo wakati akifanyiwa kitendo hicho hivyo alikosa pumzi wakati akifanyiwa unyama huo.

Kamanda huyo alisema hata hivyo mtoto huyo alifariki katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni alipokuwa akitibiwa na kwamba baada ya uchunguzi wa kidaktari na uchunguzi wa Polisi, mwili wa mtoto huyo ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

“Kwa sasa mtuhumiwa Hamimu Saidi anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Kigoma wakati upelelezi ukiendelea ili taratibu za kumfikisha mahakamani zifanyike na kwamba anatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi huo utakapokamilika,” alieleza Kamanda Mtui.
machupatom.blogspot.com

Rais Mugabe Asema Anarogwa,,,,,,,,,,,,,

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa mika 92, anazungumzia kuhusu kustaafu , lakini swali ambalo bado watu wanahoji ni ikiwa kweli anamaanisha hilo.

Mwishoni mwa juma Bwana Mugabe aliuambia mkutano wa watu wapatao 400- walio piagania uhuru kwamba ikiwa atastaafu anapaswa kupewa fursa "inayofaa" kufanya hivyo.

Pia aliwakosoa baadhi ya viongozi wa chama chake cha Zanu-PF kwa kumuombea afe na kujaribu kumroga ili wachukue nafasi yake.

Malumbano ya ndani kwa ndani miongoni mwa wafuasi wa chama tawala ya kutaka kumrithi Bwana Mugabe yameongezeka huku kiongozi huyo akionekana kuendelea kudhoofika zaidi.

Lakini si mara ya kwanza Kwa Bwana Mugabe kuongelea kuhusu kuachia madaraka it's
Mwaka 2006 alitangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008.

Licha ya hayo aligombea na kushinda katika uchaguzi uliokuwa na ghasia ambao matokeo yake yalibishaniwa.

Kwa hivyo haijawa wazi ni lini , kama kweli Rais Mugabe ataondoka madarakani.
Mnamo mwioshoni mwa juma kamati za kikanda za chama tawala cha, Zanu-PF provincial zilimuidhinisha kama mgombea wake katika uchaguzi wa 2018 , ambapo atakuwa na umri wa miaka 94.

Chama hicho kitaidhinisha uamuzi huo katika mkutano mkuu wa chama utakaofanyika mwezi ujao.
Kwa hiyo kwa sasa haionekani kama kweli anaangalia uwezekano wa kustaafu.
machupatom.blogspot.com